Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil inahitimisha mradi wa Muiin Thaqalaini wa uboreshaji na maendeleo

Maoni katika picha
Ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanywa hafla ya kuhitimu kwa washiriki wa mradi wa Thaqalaini wa uboreshaji na maendeleo, unaolenga kuandaa walimu wa Qur’ani kupitia Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya mradi wa Majmaa ya Qur’ani.

Hafla ya kuhitimisha imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na rais wa Majmaa ya Qur’ani Dokta Ahmadi Sheikh Ali, amepongeza juhudi za Maahadi kwa kufanya semina hizi muhimu, akasisitiza namna Majmaa ya Qur’ani inavyo tilia umuhimu swala la kuandaa mubalighina na wasomi wa kitabu kitakatifu wenye jukumu la kufundisha nuru ya kitabu hicho na kutumikia jamii.

Baada yake ukafuata ujumbe wa mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu shekhe Jawadi Nasrawi, ameongoe kuhusu misingi ya maendeleo katika Qur’ani tukufu, na hadithi za Ahlulbait (a.s) na kutoa Ushahidi wa aya za Qur’ani tukufu na riwaya za kizazi kitakatifu, akamaliza kwa kushukuru tawi la Maahadi ya Baabil na wakufunzi wa semina, kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuelimisha washiriki.

Naye ustadhi Hasanaini Abaka mkufunzi wa semina ya kuandaa wafundishaji (TOT) akasema katika ujumbe wake wa kufunga semina: “Masomo yamedumu kwa muda wa siku kumi mfululizo, saa (90) za masomo, wanafunzi (19) wamefaulu vizuri katika jumla ya wanafunzi (24), wanafunzi hao wanaweza kufundisha kwa ustadi mkubwa hivi sasa”.

Katika hafla hiyo tawi la Maahadi katika mkoa wa Baabil, limeonyesha mkakati wake wa mwaka (2022m), ulio wasilishwa na kiongozi wa tawi hilo Sayyid Muntadhiri Mashaikhi, amefafanua mambo mengi kuhusu Qur’ani tukufu, pamoja na huduma zinazo tolewa na Maahadi katika uwanja wa kuhifadhi Qur’ani.

Hafla ikahitimishwa kwa kuwapa vyeti wahitimu, na walimu wao wakapewa vyeti vya kuwashukuru na kuwapongeza.

Kumbuka kuwa mradi umefanywa kwa ajili ya kuandaa walimu wa Qur’ani tukufu wenye jukumu la kulea binaadamu na jamii na kuwaelekeza katika misingi ya Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: