Kitengo cha Dini kimehitimisha semina ya utamaduni awamu ya kumi na moja

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kupitia idara yake ya Tablighi, kimehitimisha semina ya utamaduni na Dini awamu ya kumi na moja, ambayo wameshiriki wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka vitengo tofauti.

Kiongozi wa Idara Sayyid Muhammad Abdullahi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kufanya semina hizo ni sehemu ya harakati ya idara yetu, tulianza miezi mingi iliyopita na bado tunaendelea, tunatarajia zitasaidia upatikanaji wa watumishi bora wanaopambika kwa maadili mema ya Dini na elimu.

Akaongeza kuwa: “Kila semina itaendelea kwa muda wa siku kumi na tano, tutaongelea maudhui zenye uhusiano na semina, zinazo husu Dini, utamaduni na elimu, pamoja na mambo yenye uhusiano na muhudumu, yanayoweza kumsaidia kuwa mfano mwema katika jamii, kila mtu anahaja ya mambo ya kidini, kifiqhi, kiitikadi, tunatarajia watanufaika nayo na watajiendeleza”.

Akabainisha kuwa: “Semina zitasimama kwa muda wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, na zitaendelea baada ya mwezi huo mtukufu, tumeandaa semina maalum itakayofanywa katika mwezi wa Ramadhani kwa watu maalum katika watumishi wa malalo takatifu”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya imekua ikifanya juhudi daima za kujenga uwezo wa wahudumu wake, hufanya hivyo kwa aina mbili, kwanza kujenga uwezo wa fani zao, na nyanja ya pili ni kuwafanya kuwa na maadili mema, kazi ya kujenda uwezo wa fani zao zinategemea na sehemu wanazotoa huduma, na semina hii ni moja ya utekelezaji wa jambo hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: