Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani kwa kusoma Qur’ani

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu Alasiri ya leo siku ya Jumapili (1 Ramadhani 1443h) sawa na tarehe (3 Shabani 2022m) imeanza kutekeleza ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani kwa kusoma Qur’ani kwa uratibu wa Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani, itakuwa inasomwa kila siku ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ushiriki wa jopo la wasomaji.

Mkuu wa Maahadi Shekhe Jawadu Nasrawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani ni miongoni mwa ratiba muhimu, imekua ikifanywa na Atabatu Abbasiyya kila mwaka, kutokana na umuhimu wa mwezi huu mtukufu, kwani ni mwezi wa Qur’ani, maghafira na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, hushuriki jopo la wasomaji mbele ya waumini na mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake inaratiba sawa na hii katika mwezi huu mtukufu”.

Akaongeza kuwa: “Usomaji wa Qur’ani unafanywa kila siku kuanzia saa kumi na moja Alasiri, kila siku linasomwa juzuu moja, imeandaliwa sehemu maalum ndani ya haram ambapo imepangwa misahafu kwa ajili ya washiriki watakao fuatilia usomaji, vimeandaliwa vipaza sauti vyenye ubora mkubwa, pamoja na jukwaa lililopambwa vizuri, wasomaji wapo watano na anasoma mmoja mmoja, wote kwa pamoja wanasoma muda wa saa moja, ratiba hiyo itaendelea mwezi mzima wa Ramadhani”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu imeandaa ratiba maalum kwa ajili ya mwezi huu mtukufu, ratiba hiyo inahusisha usomaji wa Qur’ani, mashindano ya kidini na mengineyo, katika Maahadi na kwenye matawi yake yaliyopo mikoani, kwa lengo la kueneza utamaduni wa usomaji wa Qur’ani yote ndani ya mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: