Rais wa chuo Shekhe Hussein Turabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Chuo hiki kila mwaka katika siku kama hizi, kimezowea kufanya ratiba ya kiibada na kitablighi kwa kutumia jukwa maalum la kimtandao”.
Akaongeza kuwa: Ratiba ya mwaka huu imekua na baadhi ya nyongeza kwa ajili ya kuhakikisha faida tarajiwa inapatikana, miongoni mwa vipengele vya ratiba hiyo ni:
- o Ratiba ya kiibada ya mwezi wa Ramadhani kwa njia ya mtandao, inajumla ya mambo yafuatayo:
- - Kusikiliza juzuu moja la Qur’ani tukufu kila siku.
- - Kusikiliza dua ya siku husika.
- - Kusikiliza dua Iftitaah.
- - Kuhuisha siku za Lailatul-Qadri.
- o Usomaji wa Qur’ani kwa njia ya mtandao:
- - Usomaji wa Qur’ani wa wanafunzi wa chuo na kuelekeza thabu zake kwa roho za wanachuoni na mashahidi wetu watukufu.
- - Usomaji wa Qur’ani wa marafiki wa mtandao maalum wa chuo wa mawasiliano ya kijamii
- o Mfululizo wa nadwa za kimtandao (njia za kurudi kwa Mwenyezi Mungu mtukufu): zitakazo endeshwa na walimu wa hauza kutoka Najafu.
- o Mashindano ya Qur’ani ya mwezi wa Ramadhani:
- - Shindano la (watafakari aya zake) la kuhifadhi maudhui za Qur’ani tukufu na hadithi/ awamu ya pili.
- - Shindano la (mimi nipo karibu) la kuhifadhi dua za Qur’ani/ awamu ya pili.
- - Shindano la (rahiqun makhtuum) la kuandika muhtasari wa vitabu/ awamu ya pili.
- - Shindano la (yaasubu Dini) la tafiti za kielimu/ awamu ya pili.
Kwa ushiriki na kuangalia kwenye mtandao wa chuo katika telegram tumia link ifuatayo:
https://t.me/Umm_albaneen_university_iq