Kuanza kwa awamu ya pili ya program ya Qawarira katika ugeni wa Mwenyezi Mungu

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza msimu wa pili wa program ya (Qawarira katika ugeni wa Mwenyezi Mungu) na itaendelea mwezi mzima wa Ramadhani, nayo ni maalum kwa wasichana tu, kuanzia umri wa miaka kumi na mbili na kuendelea.

Makamo kiongozi mkuu wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Awamu ya pili inafanywa baada ya mafanikio yaliyo shuhudiwa katika awamu zilizo pita, program hii inafanywa kwa njia ya mtandao, kupitia mitandao maalum ya mawasiliano ya kijamii, ratiba yake imeandaliwa na kamati ya wataalamu na inaendana na umri wa washiriki kwa kuzingatia kunufaika na mwezi huu mtukufu”.

Akabainisha kuwa: “Program inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ni:

  • - Usomaji wa Qur’ani tartiil kila siku zujuu moja.
  • - Usomaji wa dua maalum za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  • - Jiko la Ramadhani, kwenye jiko hilo kinapikwa chakula cha kiiraq.
  • - Visa na mazingatio, katika kipengele hicho hutolewa visa vya kweli vyenye mazingatio, kama visa vya mitume na umma zilizo tangulia.
  • - Mambo mbalimbali ya kiafya, kimaadili na mengineyo”.

Akasisitiza kuwa: “Tunatarajia kunufaika na mwezi mtukufu wa Ramadhani katika program hii, unaweza kushiriki kupitia link ifuatayo: https://t.me/+lQ6WHFBNKDJhOGE”.

Kumbuka kuwa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya huwa na ratiba maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kila mwaka, yenye vipengele mbalimbali, ili kupanua wigo wa program hii mwaka huu, imeamua kutumia majukwaa ya kimtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: