Usiku wa jana Jumapili siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika mkoa wa Baabil, zilianza shughuli za kongamano la Nuraini la usomaji wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani.
Hafla ya ufunguzi imefanywa ndani ya mazaru ya Alawiyya mtukufu binti wa Imamu Hassan (a.s), ilikua na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na usomaji wa Dokta Raafiy Al’aamiriy, ukafuata ujumbe wa mazaru maalum ya Alawiyyah, ulio wasilishwa na makamo katibu mkuu Ustadh Abbasi Alkafaji, akakaribisha wageni na akasisitiza umuhimu wa ushirikiano.
Ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, uliowasilishwa na mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu Shekhe Jawadi Nasrawi, akashukuru wasimamizi wa ratiba hii kubwa hapa Iraq, aidha akafafanua namna Atabatu Abbasiyya inavyo jitahidi kufanikisha miradi yake, ikiwemo program hii muhimu katika nyanja ya Qur’ani na mkoa wa Baabil kwa ujumla.
Ikafuata filamu iliyo onyesha vipengele vya kongamano kisha yakasomwa mashairi, ikahitimishwa kwa kaswida iliyosomwa na mhudumu wa Jawadaini Mula Karari Alkadhimi iliyo husu kuipenda Qur’ani na kizazi kitakatifu.
Kumbuka kuwa mradi unasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya na uongozi maalum wa mazaru ya Alawiyyah mtukufu binti wa Imamu Hassan (a.s), ukihusisha usomaji wa Qur’ani tukufu unaofanywa na wasomi wa kitaifa na kimataifa, na mashindano ya Qur’ani ya vikundi, na mashindano ya mashairi, nadwa, vikao vya usomaji wa Qur’ani na mambo mbalimbali yanayohusu Ramadhani.