Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimesherehekea siku ya kimataifa ya maktaba katika hafla iliyoratibiwa na kituo cha misingi ya kujifunza (kwenye maktaba kuu) ndani ya ukumbi wa Imamu Almujtaba (a.s) katikati ya eneo la chuo, wameshiriki walimu, wanafunzi, watumishi na wengineo, chini ya uhadhiri wa makamo rais wa chuo upande wa taaluma na utawala.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha bibi Aliya Alhuzami msaidizi wa mkuu wa maktaba ya chuo akaongea, alianza kwa kukaribisha wageni watukufu na wahudhuriaji, akataja hatua muhimu ambazo maktaba imepitia hadi ikafika hapa ilipo leo, na malengo ya baadae.
Baada yake ukafuata ujumbe elekezi kwa wanafunzi katika kuwahimiza kufikia mafanikio, uliotolewa na mkufunzi msaidizi Dhwalaal Faaiq Azubaidi kutoka kitengo cha maelekezo ya nafsi katika chuo kikuu cha Al-Ameed, ukafuata mhadhara uliotolewa na Dokta Swalehe Hasanawi, kisha akaongea Dokta Ghazwah Tamimi na Dokta Iqbaal Abul-Hubi.
Hafla ikapambwa na igizo lililofanywa na wanafunzi, na mwisho wadau wa maktaba wakapewa zawadi, nao ni wanafunzi wa chuo ambao huingia maktaba mara kwa mara.
Halafu wahudhuriaji wakaelekea kwenye ufunguzi wa maonyesho ya upangiliaji wa maktaba yaliyo andaliwa na walimu pamoja na wanafunzi wao, aina mbalimbali za upangaji wa maktaba zimeonyeshwa.