Idara ya Tahfiidh katika Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya imeratibu usomaji wa Qur’ani tartiil kwa kuhifadhi katika mwezi wa Ramadhani, kwa kushirikiana na kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f).
Kikao cha usomaji wa Qur’ani kinafanywa kila siku saa (2:30) jioni, kwa ushiriki wa wanafunzi wa kuhifadhi katika Maahadi.
Kikao cha usomaji wa Tartiil kwa kuhifadhi ni sehemu ya ratiba ya Maahadi katika mwezi wa Ramadhani, inayo lenga kutoa nafasi kwa wanafunzi kuonyesha uwezo wao.
Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu na matawi yake ya mikoani hufanya program mbalimbali katika mwezi wa Ramadhani, ikiwa ni pamoja na usomaji wa Qur’ani tartiil, nadwa za kielimu, mashindano ya mwezi wa Ramadhani na hafla za mambo yanayo husu Qur’ani.
Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu kupitia matawi yake ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajukumu la kufundisha Qur’ani tukufu na kuchangia katika kuandaa jamii yenye uwelewa wa mambo ya Qur’ani katika sekta zoto.