Idara ya usomaji katika Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, inafanya vikao vya kufundisha usomaji wa Qur’ani kwa kushirikiana na idara ya masayyid wanaotoa huduma katika Ataba tukufu.
Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinafanywa baada ya swala za Adhuhuri na Alasiri ndani ya haram tukufu ya Abbasi, chini ya usimamizi wa kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi Ustadh Alaau-Dini Alhamiri, kila siku linasomwa juzuu moja pamoja na kutoa maelekezo kuhusu usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwau wanaoshiriki kwenye vikao hivyo.
Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu kupitia matawi yake ya mikoani inafanya ratiba maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Maahadi ya Qur’ani na matawi yake yote ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajukumu la kufundisha Qur’ani na kuandaa jamii yenye uwelewa wa Qur’ani katika sekta zote.