Kuendesha vikao vya usomaji wa Qur’ani katika wilaya ya Hindiyya

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendesha vikao vya usomaji wa Qur’ani hapa wilayani.

Maahadi inashiriki kwenye vikao (35) vya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani, ambapo wasomaji mahiri wa Qur’ani wanashiriki kusoma mbele ya kundi la waumini.

Vikao vya usomaji wa Qur’ani vimepata muitikio mkubwa wa waumini, kuna vikao vya usomaji wa Qur’ani vya vijana wadogo na watu wazima.

Wanaanza kusoma kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti katika wilaya, nayo ni sehemu ya ratiba ya mwezi wa Ramadhani inayo lenga kufundisha Qur’ani tukufu katika maeneo tofauti ndani ya jamii.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu na matawi yake yaliyopo mikoani yanaprogram nyingi za mwezi wa Ramadhani, ikiwa ni pamoja na usomaji wa tartiil, nadwa za kielimu, mashindano ya Ramadhani na vikao vya usomaji wa Qur’ani.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, chenye jukumu la kufundisha Qur’ani tukufu na kusaidia kuandaa jamii yenye uwelewa wa Qur’ani katika kila nyanja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: