Ataba mbili tukufu na uwanja wa katikati yake ni sehemu ya kufanya ibada katika usiku wa Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Maoni katika picha
Malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kila siku ya Ijumaa huwa na idadi kubwa ya mazuwaru, imekua desturi ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait kufanya hivyo, kutokana na utukufu wa eneo hilo takatifu unaotajwa katika riwaya nyingi.

Alkhamisi hii ambayo ilikua na usiku wa Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, uwanja na korido za Ataba mbili tukuhu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na sehemu ya katikati yake wamefurika mazuwaru wakifanya ibada katika usiku huu mtukufu.

Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) toka mchana baada ya Adhuhuri ya leo, idadi kubwa ya mazuwaru imeshuhudiwa, na wamekua wakiongezeka hadi wakadi wa magharibi na Isha.

Wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya kazi kubwa ya kuweka mazingira mazuri kwa mazuwaru ya ufanyaji wa ziara.

Tambua kuwa huu ni usiku wa Ijumaa ya kwanza katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, mazuwaru wamefurika katika malalo mawili takatifu mwaka huu baada ya jambo hilo kukosekana katika miaka miwili iliyopita kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona.

Kamera ya mpigapicha wa Alkafeel inatuletea picha za mazuwaru hao watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: