Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatoa zaidi ya sahani (8000) za futari kwa waliofunga, wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Rais wa kitengo cha mgahawa Mhandisi Aadil Hamami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ya kugawa futari kwa mazuwaru wiki nzima kila siku, pamoja na kugawa chakula cha daku, hususan katika siku za Ijumaa ambazo huwa na idadi kubwa ya mazuwaru”.
Akaongeza kuwa: “Utaratibu uliowekwa na mgahawa katika mwezi wa Ramadhani mtukufu, na kujipanga kwa utaratibu huo, unahusu kuwajulisha mazuwaru wote kuwa watapewa futari, kila siku tunagawa karibu sahadi (3000) za futari”.
Akaendelea kusema: “Siku za Ijumaa za mwezi huu mtukufu, tunagawa zaidi ya sahadi za chakula (5000), hiyo ni idadi kubwa zaidi ya chakula tunayo toa kwa siku”.
Akabainisha kuwa: “Chakula huandaliwa mapema na wahudumu wa kitengo, tena kwa kuangalia aina za vyakula vinavyo pendwa na mazuwaru, na kutoa fursa kwao ya kutabaruku na chakula cha mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akamaliza kwa kusema: “Tutaendelea kutoa huduma hii siku zote za mwezi huu mtukufu, kiwango kitaendelea kuongezeka kila siku hadi katika siku za Lailatul-Qadri Insha-Allah”.