Vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani vimeikutanisha Maahadi ya Qur’ani ya Najafu na Madrasa ya Qur’ani ya Bagdad

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imepokea wageni kutoka Madrasa ya Qur’ani ya Bagdad, kwa lengo la kuimarisha ushirikiana baina yao na kufanya kazi kwa pamoja katika kutumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu (a.s).

Baada ya kukaribisha wageni na kuwapa maelezo kwa ufupi kuhusu harakati zinazofanywa na Maahadi, kikafanywa kikao cha usomaji wa Qur’ani tukufu, ambapo wameshiriki wasomaji wa Maahadi na wasomaji kutoka kwenye Madrasa tajwa.

Hafla hiyo imehusisha wahitimu wa semina ya kitaifa ya kwanza ya usomaji wa Qur’ani kwenye luninga (tv), aliyeanza kuburudisha masikio ya wahudhuriaji alikua ni msomaji bwana Hassanaini Miqdadi, vikafuata visomo vya wanafunzi wengine wa Madrasa ya Qur’ani.

Baada ya hapo ukafuata muhadhara uliotolewa na Ustadh Ali Akram kutoka Maahadi ya Qur’ani tukufu uliyokua ukisema (Urafiki katika Qur’ani tukufu), ameongea mambo mengi kuhusu rafiki na vigezo vyake na jinsi anavyoweza kumuathiri Rafiki yake, akatoa ushahidi wa aya za Qur’ani na hadithi za Mtume na baadhi ya shuhuda za mazingira tunayoishi katika zama hizi, akasisitiza ulazima wa kuchagua Rafiki mwema na athari yake katika jamii.

Kikafuata kipengele cha kuhifadhi Nahju-Balagha, mwanafunzi wa Maahadi ambaye ni mmoja wa mahafidhu wa Qur’ani akasoma baadhi ya maeneo katika Nahaju-Balagha, mwisho kukawa na kipengele cha maswali kuhusu Imamu Mahadi, na kikao kikahitimishwa kwa kutoa zawadi kwa washindi.

Mwisho kabisa wageni wakatoa shukrani kwa Maahadi na wahudumu wake kutokana na makaribisho mazuri waliyopewa, wakahimiza umuhimu wa kudumisha mawasiliano baina yao, kwa kufanya harakati za Qur’ani kwa ushirikiano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: