Kuendelea kwa shughuli za kongamano la Multaqa-Nurain la Qur’ani

Maoni katika picha
Shughuli za kongamano la Multaqa-Nurain la Qur’ani na kielimu katika mwezi wa Ramadhani katika mazaru ya Alawiyyah Sharifah bint Imamu Hassan Almujtaba (a.s) mkoani Baabil.

Kuna mashindano ya usomaji wa Qur’ani na mambo ya utamaduni, mbele ya mazuwaru na waumini wanaohudhuria kila siku kwenye kongamano hili la kwanza katika mji wa Baabil.

Mjumbe wa kamati ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na msimamizi wa kitengo cha Majmaa ya Qur’ani Dokta Abbasi Mussawi alipo tembelea kongamano hilo, amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika kongamano hilo, akasifu kuzi kubwa inayofanywa na Maahadi katika mkoa wa Baabil.

Akamshukuru katibu maalum wa mazaru ya Alawiyyah Sharifah Ustadh Munaadhil Ali Hassan, kwa kazi kubwa anayofanya ambayo ni daraja la ushirikiano kati ya pande mbili.

Tambua kuwa kongamano linahudhuriwa na watu wengi wanaokuja kufanya ziara kwenye malalo hiyo tukufu, na kuchota fadhila za Qur’ani tukufu patika ratiba ya usomaji wa Qur’ani kwa kuangalia na kwa kuhifadhi, Tafsiri na hadithi za Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kuwa mradi huu unafanywa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na uongozi maalum wa Mazaru ya Alawiyyah Sharifah bint Imamu Hassan (a.s), linahusisha usomaji wa Qur’ani tartiil, ambapo watashiriki wasomi wa kimataifa na kitaifa, mashindano ya Qur’ani ya vikundi, mashindano ya mashairi na nadwa za kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: