Kuanza awamu ya pili ya shindano la kijana wa Alkafeel la mwezi wa Ramadhani kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Idara ya mahusiano ya vyuo na shulechini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya jioni ya siku ya Jumamosi, imeanza awamu ya pili ya shindano la kijana wa Alkafeel la Ramadhani kwa njia ya mtandao, shindano maalum kwa wanafunzi wa chuo na sekondari.

Kiongozi wa idara ya harakati za vyuo vikuu Ustadh Muntadhir Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano linalenga kuongeza hazina ya elimu na utamaduni kwa kundi hili, kwa kujibu maswali ya shindano yanayo husu namna ya kunufaika na mwezi huu mtukufu”.

Akabainisha kuwa “Shinano linamaswali mengi ya (kidini, kitamaduni, kielimu na kihistoria), unaweza kushiriki kwa kupitia link ifuatayo (https://alkafeel.net/cont) baada ya kufungua link hiyo utatakiwa kujaza fomu maalum, kisha utaanza kujibu maswali, ukipata changamoto yeyote unaweza kutuandikia kupitia ukurasa maalum wa mradi wa kijana wa Alkafeel https://www.facebook.com/AlKafeel.Youths/ tutaendelea kupokea majibu hadi tarehe ishirini na nane ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani”.

Akafafanua kuwa: “Washindi (30) baada ya kupiga kura kwa wenye majibu sahihi watapewa zawadi, majina ya washindi yatatangazwa usiku wa Iddi Insha-Allah”.

Kumbuka kuwa shindano hili ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, na muendelezo wa mashindano yaliyo tangulia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: