Hivi karibuni kituo cha kuhuisha turathi chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa toleo ka kumu la jarida la (Alkhizaanah).
Mkuu wa kitengo cha wahariri wa jarida hilo Ustadh Muhammad Wakiil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Toleo hili ni muendelezo wa matoleo yaliyopita, toleo linamilango mitano yenye tafiti za kielimu kumi na mbili, kuna mlango wa (tafiti za turathi) wenye tafiti sita mbalimbali, na mlango wa (nakala hakikiwa) kuna tafiti tatu za uhakiki wa nakala-kale na mlango wa (matokeo ya turathi) inatafiti moja ya kielimu, na mlango wa (faharasi za nakala-kale na uwazi wa machapisho) unatafiti mbili za kielimu”.
Akaongeza kuwa: “Mlango wa (Habari za turathi) ni miongoni mwa kazi zinazofanywa na idara ya wahariri, umeingizwa kwenye orodha ya anuani za vitabu vya turathi vilivyo chapishwa hivi karibuni katika ulimwengu wa kiarabu na kiislamu”.
Akafafanua kuwa: “Utofauti katika mada za kielimu unaendana na utofauti wa kijografia kwa watafiti walioshiriki, wapo waliokuwa Misri, Saudia, Kuwait, Sudani na Hispania, jambo lisilokua na shaka kukubalika kwa jarida ni dalili ya wazi kuwa linaenda katika muelekeo sahihi na mada zake zinafaa”.
Kumbuka kuwa jarida la (Alkhizaanah) linachapishwa na kituo cha kuhuisha turathi chini ya maktaba na Daru-Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, nalo ni jarida la kielimu linalo andika kuhusu turathi na nakala-kale, linahusika na kusambaza elimu na nakala zilizo hakikiwa sambamba na kuangalia kasoro zinazo tajwa kwenye turathi na nakala kale.