Mkuu wa kituo Shekhe Saadi Shimri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ratiba hii imekua ikifanywa kila mwaka katika nchi kadhaa za Afrika, lakini mwaka huu tumeongeza idadi ya nchi na maeneo, sambamba na kupanua ratiba ya mwezi mtukufu wa Ramadhani”.
Akaongeza kuwa: “Ratiba inatekelezwa chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na baraka za kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, inavipendele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:
- - Usomaji wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani.
- - Mihadhara inayohusu mambo ya kifiqihi yanayo husiana na hukumu za funga, pamoja na mambo mengine.
- - Mihadhara ya kidini (Fiqhi, Akhlaqi, Aqida).
- - Kusoma ziara ya Maimamu watakasifu (a.s) na dua za mwezi wa Ramadhani.
- - Kuhuisha siku aliyozaliwa Imamu Hassan (a.s).
- - Kuhuisha siku aliyouawa kishahidi kiongozi wa waumini (a.s).
- - Kuhuisha siku za Lailatul-Qadri (19, 21, 23).
- - Kutoa futari kila siku kwa washiriki wa ratiba hiyo.
Pamoja na ratiba zingine za mwezi wa Ramadhani, ratiba yote inaendeshwa na wanafunzi wa Dini chini ya usimamizi wa kituo”.
Akabainisha kuwa: “Nchi zinazo tekeleza ratiba hii ni: Senegali (Dakaa na Zighinshur), Jamhuri ya Mali (Bamako), Ghana (Akra), Maulitania (Nawakshut), Kamerun (Fumbutu), Jamhuri ya Benin (Burughubarako), Seraliyon (Dafiilhol), Naijeria (Kanu-kathina), Naija (Niyami), Tanzania (Dar es salaam na Kigoma)”.
Kumbuka kuwa kituo cha Dirasaat-Afriqiyya kwenye kila msimu wa kiibada huandaa ratiba inayo husu msimu huo, sambamba na kuendeleza mawasiliano na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika bara hili, kwa kuadhimisha matukio mbalimbali.