Kuanza kwa program ya (wanahubiri) kwa ushiriki wa wahubiri 30 kutoka mikoa minne ya Iraq

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu, chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imeanza kutekeleza program ya wahubiri ya kwanza, iliyopewa jina la (wanahubiri) kwa ushitiki wa wahubiri 30 miongoni mwa wanafunzi wa Dini kutoka mikoa minne ya Iraq chini ya mkakati maalum wa tablighi.

Mkuu wa Maahadi Ustadh Muhandi Almayali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Programu hii inatokana na kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo (Ambao wanahubiri ujumbe wa Mwenyezi Mungu na wanamuogopa yeye, wala hawamuogopi yeyote ispokua Allah na anatosha Mwenyezi Mungu mhesabu), kwa ajili ya kunufaika na mwezi huu mtukufu”.

Akaongeza kuwa “Siku za nyuma tukifanya kongamano la Qur’ani la kwanza kwa wahubiri (mubalighina), walishiriki walimu wa hauza walibadilisha uzowefu wa uhubiri (Tablighi) sambamba na kufanya warsha ya mbinu za mawasiliano na uwasilishaji, na mengineyo yanayo weza kumsaidia muhubiri kuufikia umma”.

Akaongeza kuwa: “Swala la uhubiri litahusisha mihadhara kumi na tano katika nusu ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwenye misikiti, husseiniyya na mazaru takatifu kwenye mikoa lengwa, italenga kutatua changamoto za kijamii na kifamilia kwa kutumia Qur’ani na riwaya za Ahlulbait (a.s), sambamba na kufanya harakati mbalimbali zinazo husu Qur’ani”.

Tambua kuwa program hii kwa mara ya kwanza ilifanywa kwenye mikoa minne ya Iraq, ambayo ni: (Basra, Dhiqaar, Misaan, Waasit), Maahadi inatarajia kupanua program hii miaka ya mbele na kuifikia mikoa mingi na idadi kubwa ya wahubiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: