Kumuokoa kijana na maradhi ya kupooza na kurejesha nguvu za uti wa mgongo kwa njia ya upasuaji

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel iliyopo Karbala, limefanikiwa kuokoa msichana mwenye umri wa miaka ishirini na maradhi ya kupooza kwa kumfanyia upasuaji wa aina yake, jambo hilo limeonyesha umuhimu wa vifaa-tiba vya kisasa vilivyopo kwenye maabara za hospitali hiyo, na nafasi yake katika kufanikisha shughuli za upasuaji.

Daktari bingwa wa upasuaji wa maradhi ya uti wa mgongo mwenye asili ya Iran, Dokta Muhammad Zaarii amesema kuwa: “Mgonjwa alikua anasumbuliwa na maumivu makali na alikua hawezi kutembea”.

Akafafanua kuwa: “Mgonjwa alikua anaelekea kwenye kupooza, vipimo vilionyesha tatizo kwenye uti wake wa ngongo”, akasema: “Tumemfanyia upasuaji wa kurekebisha uti wa mgongo na kupandikiza ute mpya”.

Akasema kuwa: “Teknolojia ya kisasa iliyopo kwenye maabara za hospitali ya Alkafeel, inamchango mkubwa wa kufanikisha upasuaji huo, ikiwemo teknolojia ya kufuatilia usalama wa uti wa mgongo ambayo husaidia kuepusha madhara yeyote yanayo weza kutokea kwenye uti wa mgongo wakati wa upasuaji”.

Akaendelea kusema kuwa: “Baada ya kumaliza upasuaji mgonjwa ameruhusiwa na kuondoka hospitalini akiwa na afya nzuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: