Mwezi kumi Ramadhani aliaga dunia mama wa waumini bibi Khadija binti Khuwailid (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi mtukufu wa Ramadhani unamatukio kadhaa ya kihistoria, kuna matukio ya furaha na huzuni, miongoni mwa matukio yaliyo umiza moyo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s), ni kifo cha bibi Khadija (r.a), aliyefariki siku kama ya leo mwezi kumi Ramadhani mwaka wa kumi wa utume, miaka mitatu kabla ya kuhama Makka kwenda Madina.

Kifo cha bibi Khadija (a.s) ni pigo kubwa kwa Mtume (s.a.w.w), kwani hakuwa mwanamke tu, bali alikua mfano wa mwanamke mkamilifu muumini aliyejitolea kila kitu kwa ajili ya Maisha ya Mtume (s.a.w.w).

Alitoa mali zake zote na heshima yake pamoja na nafsi yake kwa ajili ya kumtumikia mbora wa binaadamu na bwana wa Manabii na Mitume, yote aliyafanya kwa ajili ya kutafuta radhi za bwana wa walimwengu na utukufu wa duniani na akhera, kutokana na uaminifu wake, Mtume (s.a.w.w) aliumia sana akawa na huzuni kubwa, ukizingatia kuwa kifo chake kilifuatana na kifo cha Ammi yake mtu aliye mnusuru mzee Abu Twalib (a.s), kutokana na ukubwa wa huzuni ya Mtume (s.a.w.w) kwao, akauita mwaka huo kwa jina la mwaka wa huzuni.

Imeandikwa katika kitabu cha Anwaaru Saatwi’a na mti wa Toba kuwa: Alipofariki bibi Khadija, Mtume (s.a.w.w) alimuandaa na kumuosha, alipotaka kumvisha sanda alikuja Malaika Jibrilu akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika Allah anakutolea salamu na anakuambia: Ewe Muhammad hakika sanda ya Khadija itatoka kwetu, hakika yeye alitoa mali yake kwa ajili yetu, Juburilu akaja na sanda, akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hii hapa sanda ya Khadija, nayo imetoka peponi Mwenyezi Mungu amemzawadia, Mtume akamvisha sanda kwa shuka yake tukufu kisha akamvisha sanda aliyoletewa na Jibriru, akawa kavishwa sanda mbili, sanda kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kutoka kwa Mtume.

Mama wa waumini bibi Khadija bint Khuwailid (r.a) jina lake ni: Khadija bint Kuwailid bun Asadi bun Abdul-Uzza bun Quraishi Asadiy, na anajina la sifa la Twahirah, alikua katika wanawake bora wa kikuraishi na wanawake wote wa Maka kwa sura na tabia, alikua na vipaji vingi, alikua na akili ya pekee, hekima na utajiri.. Shekhe Majlisi ameandika kuwa bibi Khadija alikua na nyumba kubwa wanayo weza kuingia watu wote wa Maka wakati ule.

Imepokewa kutoka kwa Ibun Abbasi, anasema: Bibi Khadija alikua wa kwanza kumuamini Mwenyezi Mungu mtukufu, watu wa kwanza kumuamini Mtume (s.a.w.w), katika wanaume Ali (a.s), na katika wanawake Khadija (r.a), alivumilia pamoja na Mtume (s.a.w.w) changamoto za utume, alikua pamoja nae kwenye shida na raha, alitoa mali zake zote kwa ajili ya uislamu, hakika alikua ni mwanamke bora wa kupigiwa mfano, hakika bi Khadija (r.a) baada ya kuolewa na Mtume (s.a.w.w) alikua na nafasi kubwa ya kumsaidia Mtume (s.a.w.w) katika kupambana na changamoto za kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu, alimpunguzia machungu aliyokua anayapata kutoka kwa makafiri wa kikuraishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: