Kamati kuu ya mradi wa Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) na kituo cha turathi za mji wa Hilla chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inatoa wito wa kuhudhuria kwenye hafla ya kumbukizi ya (Allamah Shekhe Abdulhussein Alhilliy) chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Hafla ya kumbukizi itafanywa katika kongamano la kumi na tano la kuadhimisha kumbukumbu ya mazazi ya mkarimu wa Ahlulbait Imamu Hassan Almujtaba (a.s), chini ya kauli mbiu isemayo: (Shekhe Abdulhussein Alhilliy ni Shekhe wa ma-adabaau na dira wa maqadhi).
Hafla hiyo itafanywa kwenye maqaam ya Radu-Shamsi katika mji wa Hilla siku ya Alkhamisi (12 Ramadhani 1443h) sawa na tarehe (14/04/2022m) saa mbili jioni pamoja na futari kwa watakao hudhuria.