Futari inatolewa na mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa nje kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa zaidi ya miaka mumi na moja, umezowea kugawa futari kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa barabara ya (Najafu – Karbala) ambao kuna mgahawa huo.

Unaendelea na kazi yake kwa kumpa chakula kila anaepitia sehemu hiyo na akakusudia kutabaruku na khairaati za malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Uandaaji wa futari hufanywa mapema hususan katika usiku wa Ijumaa, ambao hushuhudia idadi kubwa ya mazuwaru wanaokuja kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), imeandaliwa sehemu maalum ya kugawa chakula kwa waliofunga katika uwanja wa mbele wa mgahawa.

Kazi ya kugawa chakula inafanywa kwa utaratibu mzuri, kila anayefika kwenye mgahawa anapata chakula anachotaka pamoja na maji baridi ya kunywa, juisi na chai.

Kumbuka kuwa futari inatolewa kila siku ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, huandaliwa kwa wingi zaidi katika siku za Ijumaa na Lailatul-Qadri, kwani siku hizo huwa na idadi kubwa ya mazuwaru, kwa kuwa barabara ya (Najafu – Karbala) ni njia kuu inayoelekea katika eneo hili takatifu, mgahawa wa nje huwa kituo kikuu cha utoaji wa huduma kwa mazuwaru katika mwezi wa Ramadhani, mgahawa huandaa futari kwa mazuwaru waliofunga.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: