Kuendelea kwa ratiba ya usomaji wa Qur’ani tartiil katika mji wa Baabil

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil kwa kushirikiana na uongozi maalum wa mazaaru ya Alawiyyah Sharifah bint Imamu Hassan (a.s) inaendelea na vikao vya usomaji wa Qur’ani tukufu katika mwezi wa Ramadhani.

Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinafanywa kila siku saa kumi na moja jioni ndani ya mazaru tukufu, kwa ushiriki wa jopo la wasomaji na idadi kubwa ya mazuwaru na waumini.

Ratiba hiyo hurushwa mubashara na runinga kadhaa pamoja na mitandao ya mawasiliano ya kijamii.

Vikao hivyo ni sehemu ya ratiba ya Nuraini, inayohusisha usomaji wa Qur’ani, mashindano, nadwa, hafla na ratiba zingine za mwezi wa ramadhani.

Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil, hufanya harakati nyingi zinazo husu Qur’ani, pamoja na miradi mingine endelevu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu na matawi yake yaliyo kwenye mikoa tofauti ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inajukumu la kufundisha Qur’ani na kuandaa jamii yenye uwelewa wa mambo yote yanayo husu Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: