Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya harakati mbalimbali za Qur’ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, ilianza tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kiongozi wa Maahadi bibi Manaari Aljaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Katika kuendeleza mwenendo wa Qur’ani na malengo ya kuanzishwa kwake matukufu, Maahadi inaendesha vikao vya usomaji wa Qur’ani na harakati zingine tofauti zinazo husu Qur’ani, ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Najafu kupitia matawi yake na vituo vyake vya mikoani”.
Akafafanua kuwa: “Ratiba ya vikao vya usomaji wa Qur’ani, imegawanyika kati ya usomaji wa Tartiil, mashindano, mihadhara ya kifiqhi pamoja na usomaji wa ufundishaji”.
Kumbuka kuwa ratiba hii ilianza tangu siku ya kwanza ya mwezi huu mtukufu na itaendelea hadi siku ya mwisho, Maahadi inalenga kunufaika na mwezi mtukufu kwa kushajihisha usomaji wa Qur’ani kwa wanawake sambamba na kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani na kuonyesha umuhimu wa kusoma Qur’ani kwa pamoja.