Shada za mauwa zimepamba dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi katika usiku wa kuzaliwa ndugu yake mjukuu mkubwa

Maoni katika picha
Dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) limepambwa na mauwa bora ya Fahari, kutokana na kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kaka yake Imamu Hassan (a.s), aliyezaliwa siku kama ya kesho mwezi kumi na tano Ramadhani, mauwa yamewekwa katika mazindira ya nderemo na vifijo kutokana na kuadhimisha tukio hilo.

Watumishi wa haram tukufu na Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya, wameweka mauwa hayo kwenye ufito wa juu na chini ya dirisha takatifu, mauwa hayo yamewekewa dawa maalum ya kuyafanya yabakie katika hali nzuri kwa muda mrefu.

Kumbuka kuwa kuna nyakati na siku maalum ambazo huwekwa shada za mauwa yenye rangi na harufu nzuri juu ya dirisha la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), miongoni mwa siku hizo ni hii ya kuadhimisha kuzaliwa kwa kaka yake Imamu Hassan (a.s), siku moja kabla ya kuadhimisha hupambwa dirisha tukufu kwa shada za mauwa yaliyo andaliwa kutoka katika vitalu vya Alkafeel, kazi hiyo hufanywa na watumishi wa idara ya kusimamia haram tukufu kwa ustadi mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: