Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuanza kwa shindano la kimtandao la wanawake lenye anuani isemayo (Mjukuu Azakiyyu), katika kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).
Kwa mujibu wa kamati inayosimamia shindano linajumla ya maswali (20) tofauti, yoto yanahusu kumbukumbu ya Imamu Hassan (a.s), yanalenga kutambua historia yake na baadhi ya mambo aliyopitia katika uhai wake, na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu na mbele ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Kamati imetoa wito kwa kila msichana anaependa kushiriki kwenye shindano hili, ajiunge kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/Bwp1JKfWw2FKiAtj9 tutaendelea kupokea majibu ya washiriki hadi tarehe ishirini na tatu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, matokeo yatatangazwa siku ya Iddi mosi, pamoja na kutoa zawadi kwa washindi watatu wa mwanzo, sambamba na kutoa zawadi kwa washindi wengine saba watakao patikana kupitia upigaji wa kura kwa wenye majibu sahihi.