Maelfu ya zawadi za kutabaruku na maua yanagawiwa kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi katika kumbukumbu ya kuzaliwa kaka yake Imamu Hassan (a.s)

Maoni katika picha
Wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kitengo cha usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wanapokea mazuwaru kwa kuwapa zawadi, maua, pipi na maneno mazuri katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Mjukuu wa Mtume Imamu Hassan (a.s).

Kiongozi wa idara ya haram tukufu chini ya kitengo tajwa, Ustadh Sataar Hashim Abdu-Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa burudisho la macho ya Mtume Imamu Hassan (a.s) ni sehemu ya harakati zinazofanywa na kitengo chetu, katika kuadhimisha tarehe za kuzaliwa kwa Maimamu (a.s), ikiwepo maadhimisho haya matukufu”.

Akaongeza kuwa: “Tumeandaa zawadi laki moja zilizo wekwa kwenye vifungashio maalum, kuna marashi ya haram, pipi na uwa, anapewa zaairu huku akiambiwa maneno mazuri ya kumpongeza kwa tukio hili, tumeanza kugawa tangu Jumamosi jioni, tunawapa mazuwaru, washiriki kwenye kikao cha usomaji wa Qur’ani na wanaokuja kuswali, kuna zawadi zingine tutagawa kesho inayosadifu tarehe ya siku aliyozaliwa”.

Jambo hili linamuitikio mkubwa, mazuwaru wamefurahi na kutoa shukrani za dhati kwa wasimamizi wa shughuli hiyo, wamesema kuwa zawadi hizo zimeweka athari kubwa katika nasfi zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: