Kituo cha turathi za Basra kimeandaa nadwa ya kielimu na kikao cha usomaji wa mashairi katika kuadhimisha kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait (a.s)

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeratibu nadwa ya kielimu na kikao cha usomaji wa mashairi katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Nadwa imefanywa kwa anuani isemayo: Mambo ya pekee kwa Imamu Hassan Almujtaba kutoka kwenye kitabu cha Tabaqaat Alkabiir cha Ibun Sa’di (aliyefariki kwaka 230h”), chini ya usimamizi wa Dokta Ali Majidi Albudairi, mtoa mada alikua ni mwalimu wa historia katika kitivo cha malezi na elimu za kibinaadamu Dokta Shukuri Naasir Abdulhassan, ameongea kuhusu utukufu wa Imamu huyo mdhulumiwa.

Nadwa imehudhuriwa na kundi la wanafunzi wa Dini na walimu wa chuo kikuu cha Basra, ambapo ameongea mambo muhimu katika maisha ya Imamu (a.s) kutoka kwenye kitabu cha Twabaqaat, kulikua na maswali mengi na michango muhimu, mtoa mada amejibu maswali yote na kufafanua zaidi pale palipohitaji ufafanuzi.

Mwisho waimbaji watatu wa mashairi wakapanda kwenye jukwaa, wakaimba shairi la kuonyesha mapenzi kwa Imamu Almujtaba (a.s), nao ni Dokta Sadam Asadiy na Ustadh Abdulhussein Abdunnabi Alhalafiy, na Ustadh Hassan Saami Abdullah, hafla ikahitimishwa kwa kugawa vitabu na kutoa shukrani kwa kila aliye fanikisha tukio hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: