Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kinafanya semina elekezi

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kinafanywa semina kwa anuani isemayo: mafunzo elekezi kuhusu makubaliano ya Aizu (10015), yaliyofanywa na shirika la Kubba la mafunzo na uelekezaji, na kushiriki kundi la wakufunzi wa kitengo, na wakufunzi kutoka kwenye vituo vya mafunzo katika hospitali ya rufaa Alkafeel na kitengo cha Habari cha Ataba tukufu.

Mkufunzi wa semina Dokta Rafidah Majbal Abdullah amesema: “Lengo la semina hii ni kuandaa wakufunzi, nayo ni semina maalum kwa walimu, wakuu wa idara na wakuu wa vitengo, na kuwafanya kua waelekezaji kwani wao ndio msingi wa taasisi za ujenzi wa jamii na kuandaa walimu”.

Akaongeza kuwa: “Semina hii imekua na ushirikiano mzuri sana kutokana na kiwango cha elimu za washiriki na uwelewa wao, semina hii inamchango mkubwa kwao wa kuboresha huduma zao”.

Kumbuka kuwa semina imefanywa ndani ya ukumbi wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu, ilikua na mada nyingi, miongoni mwa mada hizo ni: uwelewa wa uelekezaji, sifa zinazo hitajika, kubaini malengo, uchambuzi wa mahitaji, kutambua darasa na masomo, ubora wa utekelezaji na ufundishaji, semina imedumu kwa muda wa siku (5) kila siku wamesoma muda wa saa (5), masomo yalikua ya nadhariya na vitendo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: