Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza kuanza shindano la kuandika Qur’ani sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).
Shindano linalenga kushajihisha utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa mujibu wa hadithi za Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), linajumla ya maswali (30) kuhusu maarifa ya Qur’ani na historia ya Maimamu (a.s).
Shindano hili ni kwa wote, wanaume na wanawake, mshiriki hatakiwi kua na umri chini ya (miaka 15), siku ya mwisho ya kupokea majibu ni siku ya sikukuu ya Iddi, saa sita usiku, unaweza kushiriki kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/MQ9wxX5JJHNq28uD6
Itapigwa kura kwa ajili ya kupata washindi (35) wenye majibu sahihi, watakao kua wameandaliwa zawadi.