Ataba mbili tukufu zinatoa pole kwa familia za wahanga wa ajali katika mji wa Baabil

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya umetoa pole na rambirambi maalum kutoka kwa wakuu wa kisheria wa Ataba mbili tukufu na watumishi wote wa Ataba hizo, kwa familia za wahanga wa ajali iliyotokea katika mji wa Tunisi mkoani Baabil, wakati wakirudi kutoka ziara kwenye malalo takatifu za Karbala.

Ugeni huo umehudhuria kwenye kikao cha kuwasomea dua watu waliopoteza Maisha kwenye ajali hiyo, kilichofanywa katika wilaya ya Jablah, na kukutana na familia za marehemu na kuwapa salamu za rambirambi.

Muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Adnani Jalukhani Mussawi kutoka kitengo cha Dini amesema: “Kwa mujibu wa maelekezo ya wakuu wa kisheria wa Ataba mbili tukufu, tumekuja kushiriki kwenye kikao cha kuomboleza na kuwasomea dua marehemu watukufu wapenzi wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), waliofikwa na umauti wakati wakirudi kutoka ziara katika siku hizi tukufu za mwezi mtukufu”.

Akasema katika ujumbe wake kwa familia za marehemu “Hakika yatupasa kuwa na subira kwa tukio hili, aidha akataja mwisho mwema wa marehem hao waliofikwa na umauti wakati wanarudi kutoka kufanya ziara, imepokewa kutoka kwa Imamu Hussein (a.s) anasema: (Atakae ni nitembelea nitamtembelea), ukizingatia walikua katika ibada tukufu ya funga, tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe na sisi mwisho mwema, Mwenyezi Mungu anasema: (Ile nyumba ya akhera tutaijaalia kwa wale wasiotaka ukubwa duniani wa ufisadi na mwisho mwema ni kwa wale wamchao Mungu)”.

Ndugu wa marehemu na washiriki wa kikao hicho cha dua wameshukuru kuhudhuria ugeni wa Ataba mbili tukufu kwenye kikao hiki cha dua, na wakaomba wasomewe dua mbele ya malalo mbili takatifu.

Kumbuka kuwa ajali mbaya ilitokea katika kitongoji cha Tunisi mkoani Baabil na kusababisha vifo vya watu kumi na moja -Allah awarehemu-.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: