Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ratiba yake ya kukutana na wanafunzi wa vyuo kila wiki, kimekutana na wanafunzi 60 wa ngazi tofauti kutoka chuo kikuu cha Mustanswariyya.
Kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo na shule Ustadh Maahir Khalidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kongamano hili ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, na tunaendelea kupokea wanafunzi kutoka vyuo tofauti, kwa kufuata ratiba maalum hadi katika mwezi mtukufu, wanafunzi wa chuo kikuu cha Mustanswariyya ni sehemu moja ya wageni wa wanafunzi tunaopokea”.
Akaongeza kuwa: “Wanafunzi hao wameandaliwa ratiba ya usomaji yenye vipengele tofauti, kulikua na kipengele cha kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kutembelea maeneo yake matukufu pamoja na kutabaruku kwa mlo wa futari katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Akaendelea kusema: “Ugeni huo umepewa mawaidha yaliyotolewa na mkuu wa kituo cha habari chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Jasaam Saidi, ameongea mada isemayo: (Utambulisho wa taifa na namna ya kuulinda) kaongea mambo mengi muhimu, kama kutambua maana ya utambulisho wa taifa, kila taifa linatunu za pekee tofauti na taifa lingine, tunu hizo ndio hutengeneza utaifa wa raia wake, hivyo ni muhimu kutambua tunu za taifa lako, aidha taifa lisipotambua tunu zake hupoteza utambulisho wako na kupoteza maana ya kuwepo kwake”.
Akabainisha kuwa: “Akaanza kutaja tunu za taifa na umuhimu wake pamoja na kusisitiza umuhimu wa wanafunzi kutambua utambulisho wa taifa lao kwani wao ndio wajenzi wa taifa”.
Khalidi akasema: “Mwisho wa mada hiyo kulikua na majadiliano ya wazi yaliyofanywa na wanafunzi na wakapewa nafasi ya kuuliza maswali, ambapo mtoa mada alijibu na kufafanua zaidi pale palipohitaji ufafanuzi”.
Mwisho wa ziara hiyo wageni wakatoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na wasimamizi wa ratiba hii maridhawa, wakaomba iendelee katika siku zijazo.