Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad chini ya Atabatu Abbasiyya, imehitimisha shindano la Qur’ani awamu ya nne, lilihohusisha usomaji wa Qur’ani kwa kuhifadhi, usomaji wa kawaida na tafsiri.
Jumla ya vikosi nane kutoka maeneo tofauti ya mji mkuu wa Bagdad vimeshiriki kwenye shindano hilo lililofanywa katika wilaya ya Husseiniyya kaskazini mashariki ya Bagdad.
Hafla ya kufunga shindano imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na ujumbe wa mkuu wa Maahadi ya Qur’ani Shekhe Jawadi Nasrawi, amewashukuru watu wote waliohudhuria na akapongeza wasimamizi wa shindano hili, akataja miradi inayosimamiwa na maahadi ya Qur’ani pamoja na matawi yake na harakati mbalimbali zinazofanywa katika mwezi huu wa Ramadhani, ikiwa ni pamoja na usomaji wa Qur’ani tartiil, nadwa za kielimu, semina, vikao vya usomaji wa Qur’ani na ratiba zingine zinazolenga kujenga uwelewa wa Qur’ani tukufu katika jamii.
Kisha usomaji wa fainali katika shindano hilo ukaanza, kulikua na mchuano mkali sana kati ya vikosi viwili cha Mauhibina na Husseiniyya Askariyyaini, hatimae kikosi cha Mauhibina kikashinda nafasi ya kwanza.
Tambua kuwa shindano hili lilianza tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, limehudhuriwa na kundi kubwa la waumini na wadau wa Qur’ani.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya na matawi yake ya mikoani, inafanya program mbalimbali za mwezi wa Ramadhani zinazo lenga kujenga uwelewa wa vizito viwili kwa raia.