Imepokewa kutoka kwa Zarara anasema, Abu Abdillahi (a.s) amesema: “Usiku wa Lailatul-Qadri unakadiriwa kuwa mwezi kumi na tisa au mwezi ishirini na moja au mwezi ishirini na tatu”.
Hivyo mwezi kumi na tisa Ramadhani inatarajiwa kuwa siku ya kwanza ya Lailatul-Qadri, siku tukufu kushinda siku zote, kufanya ibada katika usiku huo ni bora kushinda miezi elfu moja, usiku huo hupangwa mambo ya mwaka mzima, hushuka Malaika pamoja na Jibrilu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hupita kwa Imamu wa zama (a.f) na wanamuonyesha mambo aliyopangiwa kila mtu.
Ibada za siku ya Iailatul-Qadri zipo aina mbili:
Kwanza: ibada kwa ujumla ambazo hufanywa siku zote tatu (19 – 21 – 23), nazo ni:
- - Kuoga: Ni vizuri uoge wakati wa kuzama jua, ili uwe tayali umesha ugo wakati wa kuswali Magharibi na Isha.
- - Swala ya rakaa mbili, baada ya Alhamdu unasona Qulhuwa-llahu saba, baada ya kumaliza swala unasema mara sabini: (Astaghfirullaha wa-atuubu ilaihi), swala hiyo inathawabu kubwa.
- - Dua ya kufungua misahafu, unachukua msahafu unaufungua na kuuweka mbele yako kisha unasema: (Allahumma inni as-aluka bikitaabika almunzali, wamaa fiihi wafiihi ismukal-akbaru, wa asmaaukal-husna wamaa yukhaafu wa yurja, antaj’alani min utaqaaika mina nnaari), kisha omba haja zako.
- - Dua ya kuweka msahafu juu ya kichwa na kutawasal kwa Mwenyezi Mungu, fungua msahafu na uuweke kichwani na useme: (Allahumma bihaqi hadhal-Qur’ani, wa bihaqi man-arsaltahu bihi, wa bihaqi kulli mu-umini madahtahu fiihi, wa bihaqika alaihim falaa ahada a’arafa bihaqika minka… hadi mwisho wa dua kama ilivyo kwenye vitabu vya dua), kisha unaomba haja yako.
- - Ziara maalum ya Imamu Hussein (a.s).
- - Kuhuisha siku hizo tatu kwa kufanya ibada.
- - Kuswali rakaa (100) katika kila rakaa baada ya Alhamdu usome surat-Tauhiid (Qulhuwallahu Ahadu) mara kumi.
Pili: Ibada maalum za usiku wa mwezi (19), nazo ni:
- - Sema mara (100): Astaghfirullaha Rabii wa atuubu ilaihi.
- - Sema mara (100): Allahumma il-an qatlata Amirulmu-uminina.
- - Soma dua: (Allahumma lakalhamdu alaa maa wahabtalii min intwiwaai maa watwaita min shahari… hadi mwisho wa dua, kama ilivyo andikwa kwenye vitabu vya dua).
- - Soma dua: (Yaa dhaa lladhii kaana qabla kulli shaiin, thumma khalaqa kulla shaiin… hadi mwisho wa dua kama ilivyo kwenye vitabu vya dua).
- - Soma dua: (Allahumma ij’al fiimaa taqdhi wa tuqadiru minal-amri almakhtuum, wa fiimaa tafruqu minal-amril-hakiim fii lailatil-Qadri… hadi mwisho wa dua kama ilivyo kwenye vitabu vya dua).
- - Soma dua: (Allahumma innii amsaitu laka abdan daakhiran laa amliku linafsii dhwaran walaa naf’aa… hadi mwisho wa dua, kama ilivyo kwenye vitabu vya dua).
- - Dua nyingine katika usiku huo imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) inasema: (Subhana man laa yamuutu, subhana man laa yazuulu mulkuhu… hadi mwisho wa dua kama ilivyo kwenye vitabu vya dua).