Kwa picha: Kuhuisha usiku wa Lailatul-Qadri ya kwanza na kukumbuka kujeruhiwa kwa kiongozi wa waumini katika malalo ya mwanae Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) jioni ya Jumatano, umefurika maelfu ya watu waliokuja kufanya ibada za Lailatul-Qadri ya kwanza (mwezi kumi na tisa Ramadhani), katika mazingira ya kiimani ambayo watu wanasoma dua, Qur’ani na kufanya ibada mbalimbali za kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.

Mazuwaru wa usiku huu mtukufu wanafanya ibada kwa wingi na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, wanaswali sunna za usiku, na kusoma dua ya kufungua misahafu, wanasoma Qur’ani na nyeradi maalum za usiku huu, wakiwa na matumaini makubwa ya kupata baraka za mwezi huu mtukufu kwa kusamehewa madhambi na kuachwa huru na moto.

Mazuwaru wanaofanya ibada katika usiku huu mtukufu wameomboleza msiba mkubwa uliotokea katika umma wa kiislamu, msiba wa kujeruhiwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib, aliyejeruhiwa kwa kupigwa upanga na mtu muovu zaidi ibun Muljim (laana iwe juu yake) katika usiku kama wa leo.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani, imeweka kipengele maalum cha kuomboleza siku hizi za kukumbuka kifo cha kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), sambamba na kuhuisha usiku wa Lailatul-Qaqri, mihadhara yote inayotolewa katika siku hizi inamzungumzia kiongozi wa waumini Imamu Ali kuanzia siku ya kujeruhiwa kwake hadi siku aliyo aga dunia, siku zote hizo tunafanya majlisi za kuomboleza na kupiga matam baada ya kumaliza mhadhara, sambamba na kuweka mahitaji yote ya lazima kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: