Kituo cha Dirasaat Afriqiyya chini ya Atabatu Abbasiyya kimefanya nadwa ya kielimu yenye anuani isemayo (Athari za uislamu kwa mwanamke na jamii ya kiafrika) kupitia mtandao wa (google meet).
Mkuu wa kituo cha Dirasaat Afriqiyya Shekhe Saadi Shimri amesema: “Tumefanya nadwa kwa kushirikiana na kituo cha kimataifa na kiarabu” akasema: “Nadwa imehudhuriwa na zaidi ya watu (93) miongoni mwao wasomi wa sekula waliobobea katika mambo ya kiafrika na kiarabu”.
Akafafanua kuwa: “Wazungumzaji wa nadwa hiyo wamewasilisha mihtasari ya mada zao kisha zikajadiliwa kielimu”.
Akabainisha kuwa: “Nadwa hizi ni fursa ya kuwatambua wasomi waliobobea matika mambo ya kiafrika na kubadilishana uzowefu na maarifa”.
Kumbuka kuwa kituo cha Dirasaat Afriqiyya chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hufanya harakati nyingi za kielimu na kitamaduni, hususan zinazo husu bara la Afrika, ikiwa ni pamoja na kufanya nadwa za kielimu kama hii.