Atabatu Abbasiyya imetenga siku tano katika siku za majlisi zake za mwezi wa Ramadhani zinazo fanywa kila siku ndani ya ukumbi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), chini ya ratiba maalum ya tukio hilo.
Majlisi za kuomboleza zimeanza kufanywa tangu siku ya mwezi (18 Ramadhani) zitaendelea hadi mwezi ishirini na mbili, zinafanywa kila siku jioni, hufunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha mhadhiri Shekhe Hassan Khalifa hupanda kwenye mimbari na kuongea mada mbalimbali, zote hulenga kumuelezea mtu bora baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) naye ni wasii wake, ndugu yake kiongozi wa waumini Ali (a.s), mada amezigawa katika siku hizo, ambapo anaongea kuhusu maisha ya Imamu Ali (a.s), sifa zake na utukufu wake, dhulma alizo fanyiwa namengineyo.
Hali kadhalika ameongea kuhusu ibada zake mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, na ushujaa wake sambamba na kusimama kwake bega kwa bega na Mtume (s.a.w.w) katika matukio mengi, ameongea Nyanja zingine pia za maisha ya kiongozi wa waumini (a.s) yaliyojaa utukufu, ibada na maadili mema.
Ratiba inahitimishwa na majlisi ya matam inayo ongozwa na muimbaji Mula Ali Basha Karbalai, kwa kusoma utenzi unao elezea kifo cha Wasii Abu Hasanaini (a.s), huku wahudhuriaji wakiwa wamejaa huzuni kubwa kutokana na ukubwa wa msiba huo kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
Tambua kuwa mihadhara hiyo inatolewa kupitia mradi wa bibi Ummul-Banina (a.s), unaosimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, harakati zake zipo mwaka mzima, huadhimisha tarehe za kuzaliwa na kuomboleza tarehe za kifo cha mwanafamilia ya Mtume (a.s), miongoni mwa matukio muhimu ni hili la kifo cha Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s).