Uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu unashuhudia majlisi za kuomboleza kifo cha kiongozi wa wanatauhidi

Maoni katika picha
Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya kinafanya majlisi za kuomboleza kifo cha kiongozi wa wanatauhidi na bwana wa mawasii Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), baada ya swala ya Alfajiri kila siku kwa muda wa siku tatu, kuanzia mwezi kumi na tisa Ramadhani hadi mwezi ishirini na moja.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumekua tukifanya majlisi hizi kila mwaka, tumechagua muda huu kwa sababu ndio muda alioshambuliwa kiongozi wa waumini (a.s) na mal-uni bun Muljim, mazuwaru wanahudhuria kwa wingi kwenye majlisi hizo”.

Akaongeza kuwa: “Mwaka huu tumekua na mhadhiri Shekhe Muhammad Ali Rikaabi, kwenye mada zake ameongea baadhi ya mambo yaliyotokea wakati wa uhai wa Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), akaeleza msimamo wake wa kibinaadamu na jinsi alivyo simama imara kunusuru Dini ya haki, ameongea mambo mbalimbali kuhusu Imamu Ali (a.s) na historia yake, akaeleza umuhimu wa kufuata mwenendo wa Imamu Ali (a.s) sambamba na mambo mengine mengi ameyasema mhadhiri wakati wa mhadhara wake”.

Akaendelea kusema: “Baada ya mhadhara huwa kunakua na matam ambayo huongozwa na muimbaji Sayyid Hussein Aali-Twa’mah na Hussein Swabaahu Karbalai na Hussein Akili, huimba kaswida zinazo amsha hisia za huzuni kutokana na msiba wa Imamu Ali (a.s)”.

Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kimeandaa sehemu maalum za kufanyia majlisi hizi, pamoja na kutengeneza majukwaa na kupanga watu wanaoshiriki kwenye majlisi hizo kwa mistari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: