Sajili jina lako kwa ajili ya kufanyiwa ibada za Lailatul-Qadri kubwa kwa niaba

Maoni katika picha
Idara ya msimu wa Rehema imetoa wito kwa kila mtu aliyopo ndani na nje ya Iraq, anayependa kufanyiwa ibada za Lailatul-Qadri kwa niaba ndani ya malalo takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi ajisajili kwenye link ifuatayo: (http://alkafeel.net/zyara).

Ibada hizo nitafanywa na Massayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya, nazo ni: ibada za usiku wa Lailatul-Qadri wa tatu, zitakazo fanywa ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kumzuru Imamu Hussein (a.s) katika malalo yake takatifu, nayo ni ibada muhimu katika usiku huo.

Ibada hizo zitafanywa sambamba na utekelezaji wa ratiba ya kiibada katika Atabatu Abbasiyya, iliyotangazwa tangu mwanzoni mwa mwezi huu mtukufu,

Kumbuka kuwa hii ni miongoni mwa ratiba kubwa ya kuhuisha siku za mwezi huu mtukufu kupitia lugha zote zilizopo kwenye mtandao wetu ambazo ni (Kiarabu, Kiendereza, Kifari, Kituruki, Kiurdu, Kifaransa, Kiswalihi, Kijerumani), ibada hizo zitafanywa ndani ya malalo takatifu za Karbala na Najafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: