Sayyid Ibun Twausi katika kitabu cha (Iqbaalul-A’maali) ameandika hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), kutoka kwa Abu Abdillahi (a.s) alimsikia anasema, wakati watu walipo muuliza:
Je! Riziki hugawiwa usiku wa mwezi kumi na tano?
Akasema: Hapana, hugawiwa katika usiku wa mwezi kumi na tisa Ramadhani, ishirini na moja na ishirini na tatu, hakika usiku wa mwezi kumi na tisa hukutana makundi mawili.
Na katika usiku wa ishirini na moja hutawanywa kila jambo tukufu.
Na usiku wa ishirini na tatu hufanya atakalo, nao ndio usiku wa Lailatul-Qadri ambao Mwenyezi Mungu anasema: (ni bora kushinda miezi elfu).
Nikasema: nini maana ya (hukutana makundi mawili)?
Akasema: Mwenyezi Mungu hukusanya mambo aliyotaka kuyatanguliza na kuyachelewesha, au aliyohukumu.
Nikasema: nini maana ya hutenganisha katika usiku wa ishirini na moja na hutekeleza usiku wa ishirini na tatu?
Akasema: hakika hutenganisha katika usiku wa ishirini na moja, hapo hufanya Albadaa, na usiku wa ishirini na tatu hutekeleza, hapo huwa jambo lile linaingia katika hatua ya mahtuum (utekeleza).