Wanafunzi wa kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu katika mji wa Najafu wanakumbuka kifo cha Qur’ani isemayo

Maoni katika picha
Wanafunzi wa kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu katika mkoa wa Najafu, chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, wanakumbuka kifo cha kiongozi wa waumini Ali (a.s), kwa kufanya majlisi ya kuomboleza msiba huo uliotokea katika umma wa kiislamu mwaka wa (40) hijiriyya.

Majlisi ya kuomboleza iliyojaa huzuni kutokana na tukio alilofanyiwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu.

Ukafuata muhadhara uliotolewa na Shekhe Qassim Janabi, ameongea Nyanja tofauti za historia na utukufu wa kiongozi wa wanatauhidi Imamu Ali (a.s), akahimiza waliohudhuria umuhimu wa kushikamana na mafundisho ya Qur’ani na kizazi kitakasifu, ambao ndio mwenendo wa Mtume mtukufu na Imamu Ali (a.s) pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s), akawahimiza kuendelea na safari yao ya kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuzingatia aya zake, kikao hiki kinatakiwa kuwa chachu ya mabadiliko.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu hufanya harakati mbalimbali zinazo lenga kutoa mafundisho ya vizito viwili vitakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: