Muhimu.. ofisi ya Marjaa Dini mkuu imetaja kiwango cha zakatul-fitri na anaefaa kupewa

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani imesema kuwa kiwango cha zakatul-fitri mwaka huu (1443h) ni elfu mbili mia mbili na hamsini (2250) dinari za Iraq, kwa mtu mmoja badala ya unga wa ngano.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa kwenye mtandao wake maalum yanasema kuwa kiwango cha zakatul-fitri ni pishi, pishi ni sawa na kilo tatu za ngano, shairi, zabibu, mchele, au kingine chochote miongoni mwa nafaka zinazopendwa na watu wa mji husika, au kutoa thamani (pesa) inayo lingana na kiwango hicho.

Ni wazi kuwa thamani ya nafaka hizo inatofautiana kutokana na kutofautiana kwa nchi na mji, hivyo kila mtu anatakiwa kuangalia thamani ya kilo moja miongoni mwa nafaka hizo katika mji anao ishi kabla ya kulipa thani ya nafaka hiyo kwa pesa.

Wanaofaa kupewa zakatulfitri ni mafakiri, masikini na wale ambao ni halali kuwapa zakatul-maali, tambua kuwa Hashimiyya hatakiwi kupokea zakatul-fitri kama mtoaji sio Hashimiyya, wala haifai kumpa zakatul-fitri yule ambaye ni wajibu kumhudumia kama baba, mama, mke na mtoto.

Masharti ya kuwajibikiwa zakatul-fitri

  • 1-
  • 2- Akili na kusalimika na kuzimia.
  • 3- Uwezo, mtu ambae sio fakiri.

Masharti hayo yakikamilika kabla ya kuzama jua la siku ya mwisho katika mwezi mtukufu wa Ramadhani hadi sehemu ya kwanza ya usiku wa Iddul-fitri, itawajibika kutoa zakatul-fitri kwa ajili ya nafsi yako na wale walio katika mamlaka yako, sawa wawe wale ambao ni wajibu kisheria kuwahudumia au sio wajibu. Muda bora wa kutoa ni baada ya kuzama jua la siku ya mwisho wa mwezi wa Ramadhani hadi kugeuka kwa jua la siku ya iddi.

Tambua kuwa pesa za zakatul-fitri sio zaka, kwa sababu zaka hii hautakiwi kulipa pesa, bali pesa hizo ni badala ya pishi (kilo tatu) za chakula, hivyo ni muhimu kuzingatia nia wakati wa kutoa zakatul-fitri, unapotoa pesa ujue kuwa unatoa pesa badala ya pishi la chakula.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: