Atabatu Abbasiyya tukufu yakaribisha watu 400 miongoni mwa mayatima na walezi wao na wanajeshi kwenye futari

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imekua mwenyeji wa kundi la mayatima na walezi wao pamoja na wanajeshi na familia zingine za wakazi wa Karbala, chini ya ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani ya kitengo cha mahusiano. Na kukaribisha watu hao wenye umuhimu mkubwa katika kulinda amani ya taifa la Iraq.

Ustadhi Samiri Kuraitwi kiongozi wa idara ya mahusiano ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu imezowea kualika mayatima na walezi wao pamoja na familia za mashahidi na vikosi vya ulinzi na usalama, chini ya utaratibu maalum uliowekwa na kitengo cha mahusiano toka siku za kwanza za mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa: “Jumla ya watu (400) kutoka makundi tuliyotaja wamekaribishwa na kuwekewa ratiba iliyokua na vipengele tofauti, ikiwa ni pamoja na kufanya ziara kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na makumbusho ya Alkafeel pamoja na kula futari katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akafafanua kuwa: “Ratiba hiyo hufanywa kwa kushirikiana na kila kundi la walengwa katika mkoa wa Karbala, Atabatu Abbasiyya hugharamia usafiri wao kwa kuwachukua kwenye vituo vyao na kuwarudisha”.

Kwa upande wake bwana Saahir Hassan ametoa shukrani nyingi kwa niaba ya familia hizo, kwa kufanywa ratiba hii ndani ya mwezi huu mtukufu, akasema kuwa ukaribisho huu unaathari kubwa katika nafsi za washiriki.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya imefanya shughuli nyingi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, sambamba na kuwapa nafasi maalum mayatima na walezi wao, hasa wayatima ambao wazazi wao walipata shahada katika kuitikia wito wa fatwa tukufu ya kujilinda, mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) hupika futari kwa ajili ya makundi ya watu mayatima na walezi wao, sawa wawe wanakaa na walezi au kwenye taasisi za kiraia zinazo tunza mayatima, chini ya ratiba maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: