Kuhitimisha vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mji wa Baabil kwa ushiriki wa wasomaji wa kimataifa

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil na mazaru ya Alawiyya Sharifa bint Imamu Hassan (a.s), imehitimisha vikao vya usomaji wa Qur’ani vilivyo fanywa chini ya ratiba ya kongamano la Nuraini.

Hafla ya kufunga vikao hivyo imeshuhudia usomaji wa wasomi wa kitaifa na kimataifa.

Hafla ilifunguliwa kwa usomaji wa Karim Mansuri kutoka Iran, akafuata Sayyid Ahmadi A’araji kisha Raaid Alqasimiy.

Halafu yakafuata mashairi yaliyosomwa na Ali Sultani, akasoma kaswita iliyokua ikihusu kuwapenda Ahlulbait (a.s), mbele ya kundi la waumini waliokuja katika mazaru tukufu ya Alawiyya Sharifa (a.s).

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani na Mazaru waliandaa kongamano la Nurain (usomaji wa Qur’ani), ambalo wameshiriki wasomi wakubwa kutoka ndani na nje ya Iraq, aidha kongamano hilo lilikua na vipengele mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: