Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimechapisha toleo la (21) la jarida la Alghadhwiriyyah na Alkhutuwah.
Majarida hayo yameandikwa na jopo la wataalamu wa turathi na yamejaa mada nyingi za aina tofauti.
Jarida la (Alghadhwiriyyah) huchapishwa na kituo cha turathi za Karbala, na jarida la (Alkhutwa) huchapishwa na kituo cha turathi za Basra, majarida yote mawili yanachapishwa na wataalamu wa kiiraq.
Majarida yote mawili yanaandika turathi za kiislamu kupitia waandishi tofauti.
Tambua kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinahusika na kuhuisha turathi za kiislamu na kuzihakiki, kuziandika na kuzitangaza, kinamakumi ya machapisho muhimu ya mada tofauti.