Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Bagdad imeandaa nadwa kuhusu historia ya kiongozi wa waumini (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad chini ya Atabatu Abbasiyya, imeandaa nadwa ya Qur’ani katika mfululizo wa nadwa zake za mwezi wa Ramadhani yenye anuani isemayo: (Qur’ani tukufu katika historia ya kiongozi wa waumini -a.s-).

Mtoa mada wa nadwa hiyo alikua ni Dokta Imaad Alkadhimiy kutoka wilaya ya Sha’abu kaskazini mashariki ya Bagdad, akaongea kuhusu aya zinazo muhusu kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).

Shekhe Alkadhimi akaeleza utukufu wa kiongozi wa waumini (a.s) na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w).

Aidha akafafanua upekee wa bwana wa mawasii na tabia njema aliyokua nayo bila kusahau kazi kubwa aliyofanya ya kulinda kitabu cha Mwenyezi Mungu na kukisambaza.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, yenye jukumu la kufundisha Qur’ani na kusaidia katika kuandaa jamii yenye uwelewa wa Qur’ani kwenye nyanja tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: