Msimamizi wa ratiba hiyo Shekhe Haidari Aaridhwi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ratiba ya mwezi wa Ramadhani katika kituo cha wilaya ya Sanjaar hupewa kipaombele na kitengo cha Dini, hufanywa kila mwaka kwa lengo la kueneza mafundisho ya Dini na kujenga uwelewa wa Dini kwa watu, sambamba na kunufaika na mwezi huu kidini na kimaadili”.
Akaongeza kuwa: “Ratiba hii inafanywa kwa mwaka wa tano mfululizo, huwa na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ni”:
- - Kufanya kikao cha usomaji wa Qur’ani tartiil kila siku juzuu moja.
- - Kutoa muhadhara wa kidini baada ya swala ya Magharibi na Isha unaozungumzia utamaduni, miongozo, malezi na tabia.
- - Kusoma dua na nyeradi za mwezi wa Ramadhani.
- - Kuhuisha matukio muhimu yaliyotokea katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kama kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s), kifo cha kiongozi wa waumini (a.s) na mengineyo.
- - Kuhuisha siku za Lailatul-Qadri (19 – 21 – 23) kwa kufanya ratiba maalum ya kiibada katika siku hizo.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu tangu ilipokonbolewa wilaya ya Sanjaar kutoka kwa magaidi wa Daesh, imekua mstari wa mbele katika kusaidia familia za watu wa Sanjaar, pamoja na kufungua vituo vya kitamaduni kwa wakazi wa wilaya hiyo, ambavyo hutoa mihadhara ya mafundisho ya Dini na mambo mengine, kwa lengo la kujenga uwelewa wa hukumu za Dini na mambo mengine ya kielimu kwa ujumla.