Kuanza kwa kazi ya kusafisha kubba takatifu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo kinacho simamia haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya jioni ya mwezi ishirini na tano Ramadhani, wameanza kazi ya kusafisha kubba takatifu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa idara inayosimamia haram Ustadh Riyaadh Khadhiir Hassan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Kazi ya kusafisha hufanywa kila wakati, safari hii tunafanya kwa sababu ya kimbunga cha vumbi kilicho tokea sambamba na maandalizi ya Iddil-Fitri, pamoja na kuiweka katika mazingira mazuri yanayo endana na utumufu wa mwenye malalo”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya usafi hufanywa kwa kufuata ratiba iliyopangwa kulingana na mabadiliko ya hali ya heya, na kuhakikisha vifuniko vya dhahabu vilivyopo kwenye kubba haviharibiki kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kuvifanya vidumu kwa muda mrefu”.

Akafafanua kuwa “Kazi ya usafi inafanywa kwa kutumia vifaa maalum ambavyo haviathiri vifuniko vya dhahabu vya kwenye kubba, kazi imeanzia upande wa mashariki mkabala na mlango wa Furaat (Alqamiy), kinyume na upande wa muelekeo wa saa, wameanzia juu kwenda chini, wameanzia pale ilipowekwa bendera ya Kubba tukufu kuelekea chini ya kubba”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: