Watumishi wa chuo kikuu cha Al-Ameed na wanafunzi wanafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Kitengo cha maelekezo ya kimalezi katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani, wanasoma juzuu moja la Qur’ani kila siku hadi mwisho wa mwezi.

Dokta Hasanaini Adnani Mussawi rais wa kitengo tajwa, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tangu kuanzishwa kwa chuo hiki kimekua kikifanya harakati mbalimbali katika mwezi mtukufu, ikiwa ni pamoja na usomaji wa Qur’ani kila siku ambapo hushiriki walimu na wanafunzi”.

Akaongeza kuwa: “Kikao cha kusoma Qur’ani hufanywa katika saa ya mwisho ya kazi ili ratiba hiyo isiathiri utelekezaji wa majukumu yao kazini, kitengo kimeandaa mahitaji yote ya lazima ikiwa ni pamona na kuweka mazingira muwafaka”.

Mussawi akabainisha kuwa: “Lengo la ratiba hii ni kunufaika na saa za mwezi huu mtukufu kwa kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, pamoja na kuchangia katika kueneza utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa wanafunzi na kukuza vipaji vya usomaji wao, aidha ni fursa ya kutafakari aya zake na kujifunza hukumu zake”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maelekezo ya kinafsi na muongozo wa kimalezi kimetenga muda wa kuhuisha mambo yote yaliyotokea katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kama vile kumbukumbu za mazazi na vifo vya Maimamu (a.s) na matukio mengine ya kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: