Zimepokewa ibada nyingi zinazo suniwa kufanywa usiku na mchana wa Ijumaa, miongoni mwa ibada hizo ni kumzuru Imamu Hussein (a.s), jambo ambalo hufanywa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), usiku wa Ijumaa katika haram ya shahada na uaminifu Karbala huwa na umuhimu tofauti ambao hawauoni ispokua wapenzi wa Imamu Hussein (a.s), unafikiri hali itakuavipi utakapokua usiku huo ni moja ya masiku ya mwezi mtukufu wa Ramadhani tena wa Ijumaa ya mwisho.
Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya baada ya Adhuhuri ya siku ya Alkhamisi mwezi ishirini na sita Ramadhani, wamekuja watu wengi kufanya ziara kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), watu wameanza kuja kwa wingi katika muda wa Alasiri na wakaendelea kuwasiri hadi wakati wa swala ya Magharibi na Isha huku watumishi wa Ataba mbili wakiimarisha ulinzi na usalama, na kuweka mazingira mazuri na tulivu.
Karibu na muda wa swala ya Magharibi na Isha wameinua mikono na kuomba dua ya kufanya haraka kudhihiri kwa Imamu wa zama na kukubaliwa ibada (Ewe Mola tukamilishie yaliyopita katika mwezi wa Ramadhani, utusamehe mapungufu yetu katika mwezi huu, tukubalie ibada zetu, wala usituadhibu kwa yale tuliyokosea, tuweke katika kundi la watu utakao wasamehe sio katika kundi la wale wasiosamehewa).